UNCCD inajiandaa kwa kongamano maalum la mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP16 utakaofanyika Disemba mwaka ujao kwa ushirikiano na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kutunga sera za kupambana na mabadiliko ya tabianchi-UNFCCC itakayokutana mwezi ujao kwenye maandalizi ya Kikao cha kilele cha mabadiliko ya tabianchi cha COP28 huko Dubai.
Kwenye mkutano wa siku 2 uliofanyika jijini Nairobi hivi karibuni, wataalam na wanaharakati walibadilishana mawazo kuhusu mbinu mujarab za kufufua mazingira yaliyoharibika na harakati wanazofanya vijijini.